Hii ni Siasa ya Tanzania kwa Uchache
Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi vya siasa uliorejeshwa katika katiba ya Tanzania mwaka 1992. Chama tawala ni Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kimetokana na muungano kati ya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shiraz Party (ASP) ya Zanzibar. Vyama vingine vya siasa Tanzania ni Civic United Front (CUF), Tanzania Labour Party (TLP), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), National Convention for Constitution and Reconstruction-Mageuzi (NCCR-Mageuzi), National League of Democracy (NLD), Democratic Party (DP), na Demokrasia Makini .