Posts

Showing posts from April 18, 2016

UFAFANUZI JUU YA UVUMI KUHUSU HALI YA MFUKO WA TAIFA WA HIFADHI YA JAMII (NSSF)

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zisizo rasmi kuhusu hali na mwenendo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba mali za Mfuko huo zimetumiwa vibaya na hivyo kuathiri mafao kwa wanachama. Taarifa hizi zimesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wa NSSF na wadau wa Sekta ya Hifadhi ya jamii kwa ujumla kwa kuhofia usalama wa wa fedha na mafao yao. Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kuwaondoa hofu wanachama wote wa Mfuko wa NSSF na Wananchi kwa ujumla na kuwahakikishi kwamba Mfuko wa NSSF upo katika hali nzuri kifedha na unaendelea kulipa mafao ya wanachama kama kawaida. Kama mnavyofahamu, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko alikwishateuliwa na anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli zote za Mfuko. Vilevile, taratibu za kupata Bodi mpya ya Wadhamini ya Mfuko huo zipo katika hatua za mwisho. Aidha, SSRA kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania kwa mamlaka waliyopewa chi...